Posti Maarufu

Sunday, November 28, 2010

'NDOA' ZA VYUONI NA MADHARA YAKE KWA WAHUSIKA

“………..nikiwa nimejipumzisha chumbani kwangu,chumba ambacho kipo mahali ambapo kwa lugha ya wenyewe tuyaita ‘Hostel’,ghafla mlango ulifunguliwa kwa kasi ya ajabu,akaingia rafiki yangu ,kabla sijauliza kulikoni  alianza kufoka na machozi yakimtoka.”Najuta sana kumpenda ‘R’,Mapenzi yetu yalikuwa yanaenda vizuri,lakini mara tu baada ya kumaliza ‘University exams’ leo hii nimemkuta na yule jamaa yake wa zamani,yule……………”
      Ni kawaida kwa kijana aliyefikisha umri wa kuamua kile anachoweza kufanya na nani na kwa wakati gani kupewa uhuru huo pasipo kuingiliwa kimaamuzi na mtu yeyote ilimradi tu sheria ya nchi inalindwa.Uhuru huu pia ni pamoja na uhuru wa kuchagua na kumpenda yeyote wa kupendeka kwa sababu zake mwenyewe,si unajua hiki ni kizazi cha ‘DOT COM’ yaani kizazi cha utandawazi,kizazi ambacho mzazi wangu aliyepo kijijini hawezi kunichagulia huko binti wa kuoa nikakubali,huu ndiyo ukweli halisi na lazima tukubaliane nao.
     Kwa wanachuo, kama walivyo vijana wengine,na hata jamii na serikali wanalitambua hilo,wanao uhuru wa kufanya maamuzi yao wenyewe,si mnajua mtu wa ‘Diploma’ au ‘Degree’ ni mtu mkubwa kifikra na hata kiumri?.Hali hii imewapelekea wasomi hawa kuchukua maamuzi ambayo siwezi kuhukumu moja kwa moja kuwa ni mazuri au mabaya kwani nitakuwa nimeingilia uhuru wa vijana kufanya mambo ambayo pengine sisi hatuwezi kujua manufaa yake kwa tathmini ya haraka haraka.
     Uhuru huu wa kimaamuzi umewafanya wanavyuo wanaoishi katika ‘Campus’ ama ‘Hostel’ waamue kuazisha mahusiano kati yao au na watu wengine wa nje ya pale wanapoishi.Ikumbukwe tu kuwa kuna mambo mengi sana yanayomzunguka mwanachuo hasa kayika maisha yake ya kimapenzi.Zipo sababu za kijana wa kiume mwanachuo kuwa na uhisiano na binti wa ‘mtaani’ ambaye si mwanachuo na zipo sababu pia kwa kijana wa kike mwanachuo kuwa na uhusiano na Mwanamume wa ‘mtaani’ asiye mwanachuo.Labda mambo hayo tutayaangalia kwa undani katika matoleo yajayo ya gazeti hili la Familia.Kwa leo tuangalie  mahusiano ya kimapenzi kati ya wanachuo.Si unajua upendo hauchagui ili mradi tu umempenda wa kupendeka?.Mahusiano haya kati ya wanachuo,mengi kati ya aya yamezaa ‘Ndoa’ za haki hasa pale wanazuoni hawa wanapohitimu Degree na Diploma  zao na kuingia mitaani lakini pia si mahusiano yote yanayodumu kwa muda mrefu na baadhi ya watafiti mbalimabali wamebainisha kuwa mahusiano haya yamechangia ‘kuporomoka’ kielimu kwa baadhi ya wahusika na hata wengine hushindwa kuendelea kabisa na masomo yao,sisi tunaita ‘Discontinuation’.Japokuwa inaweza kuwa ni asilimia ndogo tu ya wanaoshindwa  kuendelea na masomo yao lakini lazima tutambue kuwa tayari serikali imewekeza kwa watu hawa kwa mamilioni ya fedha za mikopo wanayopewa.
    Mtafiti mmoja aliyefanya uchunguzi katika vyuo kadhaa hapa nchini,alibainisha kwamba kati ya asilimia arobaini na tisini  na saba ya wanachuo wako katika mahusiano ya kimapenzi ,na kati ya hao,asilimia hamsini hadi sabini wana mahusiano ya kimapenzi kati yao kwa wao na ni asilimia 0.5 hadi 2 tu ndio wanaodumu katika mahusioano hadi mwisho wa masomo yao chuoni na hatimaye kuoana kabisa.Si vibaya kabisa kuwa katika mahusiano ,suala kubwa hapa ni kuwa nini faida au hasara ya mahusiano haya hasa katika nyakati hizi za Ukimwi?
 Mtafiti mwingine alibainisha kuwa kila mwaka takribani asilimia moja hadi tano ya mabinti wanachuo wanapata mimba.Baadhi yao hujifungua na kuendelea na masomo yao na wengine hatujui mimba hizo zinapoishia kwani hatimaye wahusika huendelea na masomo.Bahati nzuri ni kwamba hakuna sheria inayomzuia binti mwenye mimba chuoni kuendelea na masomo si unajua wengine ni wake za watu.
     Faida kubwa zilizoelezwa za kujiingiza katika mahusiano haya zimetajwa kuwa ni pamoja na kupata misaada ya kielimu hasa mitihani inapokaribia na misaada ya  kifedha hasa pale zile za mkopo ‘Boom’ zinzpoisha,kupata  mwenza wa kukuliwaza na kukupa moyo hasa masomo yanapokuwa magumu na kupunguza ‘Academic stress’,kuepuka upweke(msononeko) na kusaidiana kumudu gharama za maisha ya chuo na wengine husema wanajiepusha na ukimwi kwa kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu na Wengine husema hii ndiyo njia ya kumpata mke au mme ambaye mnafahamiana na kuzoeana kwa muda mrefu hasa ukiwa katika uhusiano imara.
    Madhara makubwa ya mahusiano haya yamegawanyika kati ya wavulana na wasichana,japo kuna madhara ya jumla kama vile uwezekanifu wa kupata magonjwa ya zinaa,Chuki ‘hate’ kati ya wanachuo hasa pale wanapochangia bwana au binti na kuna ushahidi wa migogoro na mizozano kadha kati ya wanachuo ambayo mingi imehusishwa na kuchangia mpenzi kama chanzo.
    Kwa wasichana mimba za mapema haziepukiki na japokuwa wengine wanavumilia na kuzilea mimba hizo hadi wakajifungua wakati huohuo wakiendelea na masomo yao kama kawaida,kwa wengine uwezekanifu wa mimba hizo kutolewa kwa wakati wowote hauepukiki hasa pale mhusika anapokwepa jukumu lake na hofu ya wazazi au wanachuo wengine kugundua.Mahusiano haya pia yamehusishwa na kuporomoka kielimu kwa mhusika hasa kutokana Stress na migogoro ya kimapenzi inapojitokeza wakati wa mitihani au mitihani inapokaribia,Kupoteza muda mwingi kulea mtoto hasa kwa wale wanaojifungua hayab yote yamepelekea kushuka kwa kiwango cha kufaulu kwa baadhi ya wasomi.
    Kwa wavulana tatizo kubwa linalijitokeza ni kuishiwab fedha mapema kabla ya muda uliopangwa na Bodi ya mkopo kwani japo mnapata mkopo uliosawa mabinti wengi hubana fedha yao hasa wakati kupata chakula na kumuachia mvulana jukumu hilo ili waweze kupata fedha ya ziada kwa ajili ya saluni  na mambo ya urembo si unajua dada zetu wa vyuo wanavyopenda kupendeza?.Madhara mengine kwa wavulana ni kuporomoka kielimu hasa mahusiano yanapovunjika.Kwa kawaida msichana anayekupenda ili apate msaada wa kielimu,uhusiano wenu huimarika pale mnapokaribia mitihani na hulegalega au hata kuvunjika kabisa mara tu mitihani inapoisha.
   Matatizo yanayopelekea kuvunjika kwa mahusiano ambayo mmoja kati ya wapenzi alimpenda mwingine kwa dhati husababisha madhara ya kiakili na hivyo magonjwa kama ‘Depression’ au Post Traumatic Stress Disoder’ Hayaepukiki ambayo huweza kuwa na matokeo mabaya sana kwa mhusika.
 Kwa mfumo huu wa maisha,maisha ya kila mtu kuamua nani wa kumpenda kwa wakati gani na wapi changamoto kubwa zinazoibuka ni kuwa nani awajibike? Wazazi ambao wako huko vijijini ambako ndiko wasomi wengi wanapotokea? Au Waadhiri ambao wajibu wao ni kutoa elimu ya ‘Degree’ au ‘Diploma’ darasani tu na sio elimu ya mahusiano?Je washauri wa wanachuo wanatimiza wajibu wao?Au ni jukumu la wanachuo hawa kutatua matatizo ambayo ni matokeo ya maamuzi yao wenyewe?.Tunaweza kujiuliza maswali mengi ambayo tunaweza tusipate majibu yake kwa haraka,labda tuwaachie hawa wasomi wenyewe kwa kuwa ni watu wazima kifikra na kimwili kuamua kusuka au kunyoa.Kwani kila mmoja anao uhuru wa kupenda au kutopenda na wanavyuo wanajua jema na baya.!!!!!!!!!
  Tukutane wiki ijayo ambayo nitakuletea makala ya kusisimua zaidi.


Imeandikwa na Mwanachama wetu

Friday, November 12, 2010

ORODHA YA MAFISADI (LIST OF SHAME)

VIONGOZI WA UMMA WALIOKO KATIKA ORODHA HII WAMEKIUKA NA/AU KUVUNJA MASHARTI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO

(Kwa Hisani ya Website ya Chadema)


KANUNI/ VIGEZO VILIVYOTUMIKA

A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI

Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma wamefanya maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya Watanzania
MISINGI YA KISHERIA/KISIASA YA ORODHA YA MAFISADI

 

 

A. KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sura ya 2 ya Sheria za Tanzania imeweka ‘Malengo Muhimu na Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali’ kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:[1]

  1. Kwamba “wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi….”;
  2. Kwamba “lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi”; na
  3. Kwamba “Serikali itawajibika kwa wananchi….”
  4. ….”

Katika kutekeleza malengo na misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali iliyotajwa, “… Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
  1. Kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
  2. Kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
  3. Kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
  4. Kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
  5. Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;
  6. Kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
  7. ….” [2]
Ibara ya 7(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeamuru kuwa “… Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote na mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii …” ya Katiba. Katiba pia imewapa viongozi wa umma “… wajibu wa kufuata na kuitii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano.”[3] Aidha, viongozi wa umma wamepewa “… wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi….”[4] Vile vile viongozi wote wa umma “watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi nay a pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”[5]
Licha ya masharti ya kikatiba yaliyotajwa hapo juu, viongozi wa umma waliotajwa katika Orodha hii ya Mafisadi walikuwa wanabanwa na masharti ya sheria nyingine za nchi yetu kama ifuatavyo:

B. SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA, 1995

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali na katika sekta ya umma. Katika kutekeleza wajibu wake, Rais anatakiwa kuweka taratibu thabiti za maadili katika utumishi wa umma ambazo:
  1. Zitahakikisha kwamba kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na wajibu wake kama kiongozi wa umma;
  2. Zitaweka taratibu za wazi za maadili kuhusu migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa;
  3. Zitapunguza uwezekano wa migongano inayotokana na maslahi binafsi kuingiliana na shughuli za umma za viongozi wa umma na kuweka taratibu za utatuzi wa migongano hiyo inapotokea.
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma:
  1. kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali;
  2. kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu;
  3. kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma;
  4. kuhusiana na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya;
  5. kuhusiana na maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma watapanga masuala yao kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma;
  6. kuhusiana na zawadi, viongozi wa umma hawatadai au kupokea manufaa ya kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo ndogo, ukarimu wa jadi/takrima au manufaa mengine yenye thamani ishara, isipokuwa tu kama manufaa hayo yatatokana na mkataba au mali ya kiongozi wa umma;
  7. kuhusiana na upendeleo, viongozi wa umma hawatatumia vyeo vyao rasmi katika kusaidia taasisi au watu binafsi katika mahusiano yao na serikali iwapo kufanya hivyo kutasababisha upendeleo kwa mtu yeyote;
  8. Kuhusiana na mali ya serikali ambayo viongozi wa umma hawatatumia ama moja kwa moja ama kisiri siri, au kuruhusu kutumiwa kwa mali ya serikali ya aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mali ya serikali iliyokodishwa kwa ajili ya kumnufaisha kiongozi wa umma;
  9. Kuhusiana na ajira baada ya utumishi wa umma, viongozi wa umma hawatafanya vitendo vitakavyoshusha hadhi na heshima ya utumishi wa umma baada ya kuondoka katika utumishi ili kupunguza uwezekano wa matarajio ya ajira kuleta migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wanapokuwa katika utumishi wa umma; kupata upendeleo baada ya kuondoka katika utumishi wa umma; kutumia taarifa zinazopatikana kutokana na utumishi wa umma kwa maslahi binafsi; na kutumia utumishi wa umma kwa ajili ya kupatia nafasi za ajira nje ya utumishi wa umma.
A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

1. DR. DAUDI T.S. BALALI

Dr. Daudi Balali amekuwa na bado ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Gavana Balali amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
  1. Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, ameruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufikia Shilingi 522, 459, 255,000 katika ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyoko barabara ya Mirambo, Dar es Salaam na Gulioni, Zanzibar. Aidha taarifa kutoka vyanzo vingine zinaonyesha kwamba mwaka 1998 kampuni ya Skanska Jensen ya Sweden ilituhumiwa kutoa hongo ya Dola za Marekani milioni 5 kwa Gavana Balali tuhuma zilizopelekea kampuni hiyo kupigwa marufuku kushiriki tenda ya ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, katika mazingira yanayoashiria ufisadi mkubwa, kampuni ya Group 5 ya Afrika ya Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Skanska Jensen ilipewa tenda ya kujenga majengo hayo ya Benki Kuu;
  2. Kufuatana na barua iliyotajwa katika aya ya (i) hapo juu, Gavana Balali aliidhinisha na/au kuruhusu na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 118,396,460.36 zilizopelekwa katika akaunti isiyojulikana ya Benki ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini kama malipo ya madeni ya kampuni muflisi ya Meremeta Ltd. iliyokuwa inachimba dhahabu katika eneo la Buhemba wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara. Kwa miaka mingi Serikali ilikuwa ikitoa taarifa za uongo kwamba Meremeta Ltd. ilikuwa ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Hata hivyo, nakala ya usajili iliyotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales inaonyesha kwamba kampuni hiyo iliandikishwa nchini Uingereza tarehe 19 Agosti 1997 na ilifilisiwa huko huko Uingereza tarehe 10 Januari 2006. Aidha, taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya tarehe 31 Mei 2005 inaonyesha kwamba Meremeta Ltd. ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania kama tawi tarehe 3 Oktoba, 1997. Vile vile taarifa hiyo inaonyesha kwamba hisa 50 za Meremeta Ltd. zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini na hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa kupitia kwa Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha. Inajulikana vile vile kwamba Gavana Balali aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Meremeta Ltd. kati ya mwaka 2004 na 2005. Hata hivyo, kuna utata mkubwa juu ya nani ni mmiliki hasa wa Meremeta Ltd. kwa kuwa taarifa ya BRELA inaonyesha pia kwamba makampuni mawili ya Kiingereza – London Law Services Ltd. na London Law Secretarial Ltd. – nayo yanamiliki hisa moja moja za Meremeta Ltd. Makampuni hayo yanatumia anwani moja iliyoko 84 Temple Chambers, Temple Avenue, jijini London. Haijulikani ni kwanini Gavana Balali aliruhusu fedha za umma kutumika kulipia madeni yote ya kampuni ambayo Serikali ilikuwa inamiliki hisa 50 tu wakati makampuni mengine ya kigeni yalikuwa yanamiliki hisa 52. Na kama ilivyosema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, uhalali wa Serikali kulipa madeni ya Meremeta Ltd. kwa Nedbank Ltd. badala ya kuiacha benki hiyo kudai malipo hayo kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na wadeni wengine haujulikani;
  3. Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu, Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kampuni ya Tangold Ltd. Katika hotuba yake Bungeni ya tarehe 27 Juni 2007, Waziri wa Madini na Nishati Mheshimiwa Nazir Karamagi alidai kwamba “… mali na madeni ya MEREMETA yamehamishiwa kwenye kampuni mpya ya TANGOLD ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.” Hata hivyo, barua ya BRELA ya tarehe 4 Julai 2007 inatamka wazi kwamba “Tangold Limited ni kampuni ya kigeni iliyosajiliwa kwa mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Mauritius, na baadae kuandikishwa nchini Tanzania kama tawi la kampuni ya kigeni.” Barua hiyo inaongeza kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania mnamo tarehe 20 Februari 2006 na kwamba Katiba ya kampuni hiyo haikuonyesha “majina ya wanahisa wa kampuni na mgawanyo wa hisa.” Barua hiyo ya BRELA inaonyesha kwamba wakurugenzi wa Tangold Limited ni pamoja na Gavana Balali, Gray S. Mgonja ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Andrew J. Chenge ambaye ni Waziri wa sasa wa Miundo Mbinu, Patrick W.R. Rutabanzibwa ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Vincent F. Mrisho ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha fomu Na. 1F inayohusu usajili wa kampuni za kigeni iliyowasilishwa BRELA na mawakili wa Tangold Limited na kusainiwa na Gavana Balali tarehe 20 Mei 2005 inaonyesha kwamba kampuni hii imetokea “Jamhuri ya Mauritius” na anwani yake iko Suite 520, Barkly Wharf, Le Caudan, Waterfront, Port Louis, Mauritius. Hivyo ndivyo kinavyoonyesha cheti cha usajili kilichotolewa na Msajili wa Makampuni wa Jamhuri ya Mauritius mnamo tarehe 5 Aprili 2005 na pia leseni ya biashara iliyotolewa kwa Tangold Ltd. Port Louis nchini Mauritius tarehe 8 Aprili 2005. nyaraka hizi pia zinaonyesha kwamba Tangold Limited ni kampuni binafsi (private company limited by shares). Kuna utata zaidi kwani kifungu cha 7(e) cha Katiba ya Tangold Ltd. kinaruhusu hisa za wanaomiliki kampuni hiyo binafsi kuhamisha hisa zao kwa wanandoa, baba, mama, watoto, wajukuu au wakwe zao wa kike au wa kiume! Sasa kama ni kweli kwamba Tangold Ltd. inamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja, je nani ni mke au mume au baba au mama au motto au mjukuu au mkwe wa kike au wa kiume wa Serikali ya Tanzania ambaye anaweza kuhamishiwa hisa za kampuni hiyo? Katika barua yake ya ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alidai kwamba Ofisi yake ilishindwa kuelewa uhalali wa malipo ya dola za Marekani 13,340,168.37 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Tangold Limited;
  4. Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia mkopo usio na riba wa Dola za Marekani 5,512,398.55 kwa kampuni ya Mwananchi Gold Co. Ltd. kati ya mwaka 2004 na tarehe 30 Juni 2006. Kati ya fedha hizo, deni la dola 2,807,920 limedhaminiwa kwa dhahabu ghafi ambayo ingenunuliwa kutokana na fedha za mkopo zilizotolewa na Benki Kuu yenyewe! Kwa maana rahisi ni kwamba kampuni ya Mwananchi Gold haijatoa dhamana yoyote inayoeleweka kwa mabilioni ya shilingi ilizokopeshwa na Benki Kuu chini ya Gavana Balali. Kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, hadi kufikia mwezi Desemba 2006 Mwananchi Gold Co. Ltd. ilikuwa imeshindwa kulipa hata riba ya mkopo huo kwa kiasi cha dola za Marekani 62,847.91. “Katika mazingira haya”, inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, “hatukuweza kujiridhisha kwamba deni la dola la Marekani 5512398.55 inalodaiwa (Mwananchi Gold Co. Ltd.) hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006 linaweza kulipika.” Je, ni kampuni gani hii iliyopewa mamilioni ya fedha za umma katika fedha za kigeni bila kudaiwa riba au kupewa kipindi maalumu cha kulipa mkopo huo? Kufuatana na taarifa za BRELA, Mwananchi Gold Co. Ltd. ni kampuni binafsi ambayo wanahisa wake ni Benki Kuu ya Tanzania yenye hisa 500, Shirika la Maendeleo la Taifa (hisa 500), Mwananchi Trust Co. Ltd. (hisa 1,123) na Chimera Co. Ltd. (hisa 500). Kampuni hii ilisajiliwa kama kampuni binafsi tarehe 12 Desemba 2002. Mawakili wake ni kampuni ya mawakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Associates ikiwashirikisha aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wakati huo marehemu Francis L. Nyalali, Waziri Mkuu wa zamani Joseph Sinde Warioba na aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa R. Mahalu. Wakurugenzi wa Mwananchi Gold ni Joseph Sinde Warioba, Gavana Daudi Balali, Col. J. Simbakalia, Vulfrida Grace Mahalu, Yusuf H. Mushi na raia wawili wa Italia, Paolo Cesari na Patrizio Magrini. Vulfrida Mahalu ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa kampuni binafsi ya VMB Holdings (1996) Ltd. na pia ni mke wa Profesa Mahalu ambaye kwa sasa anakabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi kutokana na madai ya wizi wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Serikali wakati akiwa balozi wa Tanzania nchini Italia! Kanali Simbakalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Taifa na Yusuf Mushi ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni binafsi ya Business Machines Consultants (T) Ltd;
  5. Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya shilingi 131,950,750,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. Vile vile Gavana Balali anadaiwa kuidhinisha malipo ya shilingi bilioni 4,228,658,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. “Katika mazingira haya”, inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, “hatukuridhika na uhalali wa hasara ya shillingi bilioni 131.9 zinazoonekana katika taarifa za fedha hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006….” Kwa mantiki hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu aliiasa Benki Kuu kuanzisha uchunguzi wa malipo yaliyosababisha hasara ya shilingi 131,950,750,000 na shilingi 4,228,658,000 zilizolipwa kama malipo ya madeni ya nje. Waziri wa Fedha Zakia Meghji mwenyewe amekiri kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma katika akaunti za malipo ya madeni ya nje katika barua yake kwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). IMF yenyewe katika taarifa kwa vyombo vya habari ya tarehe 27 Juni 2007 imetamka kwamba “Serikali (ya Tanzania) imekwisha kusimamisha malipo kutoka akaunti hiyo hadi uchunguzi huo utakapokamilika.” Wakati Serikali ikitoa taarifa hizi kwa IMF imekataa kata kata kutoa taarifa hizi kwa umma wa Watanzania wala wawakilishi wao Bungeni.
A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

2. ANDREW J. CHENGE

Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya sasa ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka yote kumi ya utawala wa Rais Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo, Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa “mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na … aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria….”[6] Katika kipindi hicho cha miaka kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
  1. Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
  2. Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
  3. Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake Bungeni tarehe 6 Novemba 2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega ulipofunguliwa hadi mwaka huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.614 wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.

3. BASIL P. MRAMBA

Mheshimiwa Basil Mramba ni Mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Rombo na Waziri wa Viwanda na Biashara na kwa miaka kumi ya utawala wa Rais Mkapa alikuwa ndiye Waziri wa Fedha. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Mheshimiwa Mramba amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
  1. Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu. Chini ya mkataba wake na Serikali ya Tanzania, Kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu. Kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart (Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi wa mahesabu ya makampuni ya dhahabu, ijapokuwa “hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu ukaguzi uliofanywa katika mwaka 2005/06”! Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alisema katika barua yake kwamba “hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani.”
  2. Vile vile kuna taarifa za kuwepo kwa rushwa na/au ufisadi mkubwa kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex Stewart Assayers. Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye jina la Bwana Basil ambaye ana wadhifa wa Waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye kampuni hiyo na kuwa analipwa na kampuni hiyo. Kwa mujibu wa Flores, hakuwezi kukawa na ushahidi wowote kuthibitisha kwamba ‘Bwana Basil’ anapokea malipo kutoka kwa Alex Stewart kwa vile malipo yote kwake yamekuwa yakifanyika nje ya nchi. Kwa kadri tunavyofahamu, mtu pekee aliyekuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Tatu na ambaye pia ni waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na ambaye ana jina la ‘Basil’ ni Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba. Tumemtaka Waziri wa Fedha kutupatia nakala ya Mkataba kati ya Benki Kuu na Alex Stewart, na kuwataka Mheshimiwa Basil Mramba na Erwin Flores walete maelezo yao kwetu kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka, Haki na Kinga za Bunge ya mwaka 1988 kwa barua yetu ya tarehe 18 Julai 2007 ili waweze kujibu tuhuma hizi. Bado tunasubiri majibu hayo.
  3. Mheshimiwa Mramba amehusishwa pia na ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za umma na uuzaji holela wa rasilmali za taifa letu. Kashfa hizo ni pamoja ni ununuzi wa rada ya kijeshi, ununuzi wa ndege ya Rais, na ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na National Microfinance Bank (NMB).

4. GRAY S. MGONJA

Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.

5. PATRICK W.R. RUTABANZIBWA

Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati mikataba mibovu ya madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Kwa sasa Bwana Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited. Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna mgongano mkubwa kati maslahi yake binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa kuyalinda akiwa kama kiongozi wa umma

6. NIMROD ELIREHEMA MKONO

Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa kampuni ya mawakili ya Mkono & Company Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali inaainisha kuwa Benki Kuu imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates wamekwishalipwa shilingi 8,128,375,237 kwa fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia 13.5 ya deni lote inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.
Lakini hoja nyingine ya kimsingi ni kama malipo haya kwa mawakili yanaruhusiwa chini ya Kanuni za Malipo ya Mawakili na Uamuzi ya Gharama za Kesi za mwaka 1991, Tangazo la Serikali Na. 515 la mwaka 1991 (Advocates’ Remuneration and Taxation of Costs Rules, 1991). Kanuni hizi zimeweka kiwango cha malipo ya mawakili katika kesi ambazo fedha inayodaiwa ni zaidi ya Shilingi milioni 10 kuwa ni asilimia tatu. Kwa kufuata masharti ya sheria hii ya malipo ya mawakili, kampuni ya Mkono & Co. Advocates ilipaswa kulipwa Shilingi bilioni 1.8.
Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme’ iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: “Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)
Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: “Mheshimiwa Spika, ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa. Nimrod Mkono alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya Marcus Ltd., makampuni ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya utaratibu wa DCP.”

7. NAZIR KARAMAGI









8. ROSTAM AZZIZ









9. EDWARD LOWASSA

10. BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba

11. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.
Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

MKUU HUYU WA DEPARTMENT YA PROCUREMENT AND SUPPLIES CBE ACHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU

Mtandao wetu umepata taarifa kuwa Mkuu wa Deaprtment ya Procurement and Supplies Management katika chuo cha CBE Bwana Mohamed amekuwa akiwanyanyasa wasichana wa kike kwa makusudi.
Bwana Mohamed amekuwa akiwasumbua wasichana wa kike kwa kuwatongoza na Pindi wanapomkaa hujenga chuki dhidi yao na kutoa alama zisizo za haki katika Mitihani yao. Kutokana na Recordings tulizonazo za maongezi yake na Baadhi ya Wanafunzi wa kike waliowasilisha malalamiko yao kwetu,imedhihirika kabisa kuwa tabia ya Mkufunzi huyu haina Maadili.
Uchunguzi wa awali tulioufanya, umedhihirisha kuwa baadhi ya Wanafunzi Wamenyanyaswa katika mitihani  kwa Makusudi na Mwalimu huyu. Tunauomba uongozi wa Chuo uchukue hatua za haraka.
Wazazi wanapowaleta watoto wao chuoni wana imani kuwa wakufunzi wataendeleza malezi mema yenye kuwajenga wanafunzi kimaadili ili kuzalisha wataalamu wenye maadili mema ya kulinjenga taifa letu na iwapo wakufunzi watakuwa ndio wa kwanza kuharibu maadili je wataalamu watakaozalishwa watakuwa na maadili gani? Na wazazi tutakuwa na imani gani dhidi ya Vyuo.
Iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa tutampleleka Mahakamani mkunfunzi huyu na kwa Ushahidi wa recordings na Picha tulizonazo itatosha kabisa kumuwajibisha mkufunzi huyu huku tukiomba Mahakama itoe kibali kwa Mitihani yote ya Wanafunzi walioferishwa isahihishwe na Mkufunzi wa nje atakayeteuliwa na Mahakama ili kudhihirisha Uonevu na Kuwalinda walioleta Malalamiko... Hatupendi kufika huko hivyo tunaamini uongozi wa CBE utachukua hatua muafaka ili kuepuka kuharibika kwa credibility ya Chuo kwa Jamii


Mwanamtanda

MTANDAO WA KUBORESHA MAADILI TANZANIA: WALIMU WA SAUT WANAWALAZIMISHA WANAFUNZI WA KIKE K...

MTANDAO WA KUBORESHA MAADILI TANZANIA: WALIMU WA SAUT WANAWALAZIMISHA WANAFUNZI WA KIKE K...: "Hii ni Barua iliyo tumwa kwa VC na DVCAA wa SAUT KUHUSU UDHALILISHAJI WA WANAFUNZI HASA WA MWAKA WA KWANZA Ndugu,'Maadili' au 'uadilifu' n..."

Thursday, November 11, 2010

POSTER YA STOP SEXUAL HARASSMENT IN UNIVERSITIES

TUNATAKA KUJUA WAUAJI WA MAALBINO WAMEFANYWA NINI

Baada ya Kampeni nyingi za Wanasiasa ambao wanajamii baadhi walisema Vigogo wanahusika na Mauaji ya Albino..kulinda nafasi zao kwa ushirikina,....................
Tunataka sasa kujua wauaji wamechukuliwa hatua gani

MAVAZI YASIYO NA MAADILI YAPIGWE MARUFUKU BUNGENI

Kama Mbunge anawakilisha Kundi fulani la Kijamii ina maana anawakilisha pia taswira ya wananchi anaowawakilisha. Nimemuona Mbunge mteule Vicky Kamata na Catherine Magige wakiwa na Vihereni Miguuni..Japo Wanajiwakilisha wenyewe lakini wanawawakilisha waliowapendekeza kwa Mkuu.. Hebu wasituchafulie Bunge letu...Bunge si Jukwaa la MITINDO. Naomba mavazi na mapambo ya kichangudoa yapigwe marufuku Bungeni ili kulinda maadili ya Bunge


Mwanamtandao

MFUMO WA MITIHANI YA VYUO VIKUU HAUTOI NAFASI YA KUWATAMBUA WENYE VIPAJI KWA HAKI

        Nilikuwa  naongea na rafiki yangu mmoja tuliyewahi kusoma naye katika shule moja ya sekondari,kwa sasa  anasoma katika chuo kuu kimoja cha afya ya binadamu  hapa nchini.Mbali na kuongelea matatizo mengi yanayojitokeza katika fani mbalimbali za vyuo vikuu, suala lililonivuta zaidi ni mfumo wa kuwatahini wanvyuo hasa katika mitihani ya mazoezi kwa vitendo.Pale mwanachuo anapofika hatua ya kufanya mitihani ya kliniki kwa upande wa wanavyuo wa vyuo vya afya ya binadamu, anatakiwa  kuchukua maelezo ya mgonjwa ili baadaye awakilishe maelezo hayo kwa yule aliyepangiwa kumsimamia ,hapo ataulizwa maswali ambayo iwapo atayajibu vema atapewa maksi kadha.Njia hii inaweza kuwa ndiyo njia bora kabisa ya kumtahini mwanachuo hasa ukizingatia kuwa inamjengea kujiamini zaidi  katika kusema na kufanya mambo.
       Tatizo kubwa linaloibuka ni tofauti kati ya watahini au “supervisor” wa zoezi hili,labda ni kwa sababu ya wingi wa wanavyuo inakuwa vigumu kwa mtahini mmoja kuwasimamia wanavyuo  wote.Hapo kitengo husika hulazimika kuweka wasimamizi zaidi ya mmoja wenye viwango tofauti vya kielimu na wanaotofatutiana katika kutoa maksi.Kwa mfano iwapo utakutana na Profesa katika mtihani andika umeumia, maana atakuulizauliza vitu vingi sana tofauti na utakapokutana na mtu mwenye degree mbili tu ama ‘specialist’ .Kutokana  na hizi tofauti kati ya watahini na kwa kuwa utoaji wa maksi ni utashi wa msimamizi binafsi hapa linazuka suala ambalo matokeo yake si mazuri kwani iwapo mwanafunzi asiye bora atakutana na specialist akampa maksi nyingi kwa utashi wake binafsi ina maana huyo atakuwa amefaulu sana na kuonekana bora.Labda utasema kama mtu ni bora atakuwa bora tu hata akikutana na Profesa lakini hoja hapa ni kwamba mpaka mtu kuitwa Profesa anakuwa anafahamu mambo mengi sana ambayo atataka umueleze kiprofesa profesa.
         Changamoto nyinyine zinajitokeza katika katika vyuo vingi ni katika kazi za ziada yaani ‘assignments’ ambazo iwapo utampata mwalimu muelewa wa hali halisi ya usomaji utapewa alama za kuchekelea.Changamoto nyinyine ni katika usahihishaji wa mitihani ya kuandika inayohitaji maelezo “essay’ ,siyo siri waulize wanavyuo wengi watakuambia iwapo mwalimu fulani atasahisha mtihani wako utakuwa na nafasi kubwa ya kufaulu na waalimu ambao wakisahisha mtihani wako utakuwa na nafasi ya kutokufaulu wanajulikana pia.
       Tatizo linalojitokeza ni kwamba kwa kuwa wanavyuo katika vyuo kadhaa  hugawanywa katika makundi na wanapangiwa walimu tofauti tofauti wa kuwafundisha ,pale mwanachuo anapokutana na mwalimu ambaye  siyo yule aliyemfundisha kama msimamizi wake katika mtihani au assignments au mitihani ya maelezo marefu (essay) ,kumekuwa na matatizo ya mgongano wa kitaaluma kwani japo elimu na mwongozo wa kielimu ni wa aina moja  lakini kila mwalimu anapenda kumuandaa mwanafunzi kwa utashi wake ambao si lazima mwalimu mwenzake akubaliane nao.
       Labda kwa kuwa watahiniwa ni wengi kuna haja ya kuweka viwango vya kumtahini mwanafunzi,viwango na maelekezo ambayo vitengo husika vitawajibika kuhakikisha kuwa vinazingatiwa katika kutahini wanavyuo la sivyo atumike mtahini mmoja tu pasipo kujali atatumia muda gani kuwasimamia au kusahihisha mitihani ya wanachuo wote wa kozi husika.
     Hii yote ni katika kujaribu kumpa kila mtu kile anachostahili kupata hasa katika utoaji wa tuzo mbalimbali vyuoni.Sisemi kila anayepewa tuzo si bora bali tumekuwa tukishuhudia minong’ono ya chini chini kati ya wanavyuo wakihoji kwa vipi mtu Fulani apewe tuzo.Actually wanavyuo wenyewe wanafahamiana ,wanajua ni nani aliyebora na ni nani asiyebora na iwapo yule ambaye wanavyuo wenyewe katika kozi na mwaka husika wanamkubali kwamba yuko ‘fit’ kimasomo akakosa kutambuliwa kwa tuzo na kupewa mwingine ambaye pengine anaonekana kabisa hayuko ‘fit’ kwa binadamu yeyote mwenye akili timilifu ni lazima atakuwa na walakini.
     Nawapongeza sana waalimu wa vyuo kwa kazi nzuri wanayoifanya.Kwani wamekuwa wakijitahidi kukabiliana na  changamoto za kuongezeka kwa wanavyuo kwa kasi kiasi kwamba wao wanabeba mzigo ambao ni matokeo ya propaganda za kisiasa za kuongeza idadi ya wanaojiunga katika vyuo pasipo kuongeza miundombinu na waalimu.Kwa kuwa suala la kuongezeka kwa idadi ya wanavyuo ni la kisiasa zaidi si ajabu kuwakuta wanavyuo wakisoma wakiwa wamesimama kwa kukosa mahali pa kukaa kutokana na wingi wao na nadhani kwa miaka ijayo wengine watakuwa wanachungulia madirishani kwa pale ambapo hali hiyo haijajitokeza.
      Lengo la makala hii ni kujaribu kueleza hali  halisi ilivyo na kutoa changamoto kwa wakuu wa vitengo vya kielimu kutafuta mbinu iliyobora kabisa ya kuwatahini wanavyuo na kuwatambua waliobora kwa haki.
      Ushauri wa bure kwa wanavyuo ni kwamba lazima kukaza buti kukabiliana na changamoto zozote zinazojitokeza katika  mfumo mzima wa elimu na mitihani.Ni vema ukajiandaa kisawasawa ili ujijengee hali ya kujiamini pasipo kujali utakutana na nani katika mtihani.Kwa kufanya hivyo utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri ya kufaulu kwa kiwango kizuri pasipo kujali utapata tuzo au la.
Nawapongeza sana wanavyuo ambao wanasoma kwa bidii sana na hatimaye kupata tuzo mbalimbali kwa kutambua vipaji na bidii zao binafsi katika elimu kwa ujumla .
                             Kaza buti na utavuna ulichopanda
                             
Mwanamtandao

ABC’ KISU KINACHOPOTEZA MAKALI KATIKA KUZUIA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

            Wakati nchi ya Uganda ilipofanikiwa kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) katika miaka ya tisini,wataalamu na watafiti waliobobea katika masuala ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya zinaa ikiwemo Ukimwi walifurika kwa wingi nchini humo ili kujua mbinu zilizotumika kupunguza maambukizi mapya kushuka kwa kasi ya ajabu.Mojawapo ya matokeo ya tafiti ambazo zilifanyika ilikuwa ni matumizi ya sahihi ya njia ya ‘ABC’ katika kupambana na maambukizi ya Ukimwi.Matokeo ambayo yalipelekea nchi nyingi kuanza kutumia mfumo huo kaatika mapambano hayo.
            ‘ABC’ ni kifupi cha maneno matatu ya kiingereza yaani ‘Abstinence,  Being faithful na Condom using) kwa Kiswahili yakimaanisha Kujiepusha kufanya ngono,Kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako na Kutumia Kondomu.ABC imekuwa ikitumika kama njia ya mapambano dhidi ya Ukimwi kwa miaka mingi sasa.Mbinu hii mbali na kuonyesha mafanikio katika nchi kama Uganda , Thailand (iliyoitwa baba wa kondomu kutokana na matumizi ya kondomu kwa kasi)  na nchi nyingine nyingi bado kuna changamoto nyingi zilizojitokeza.
              Changamoto nyingi sana zimejitokeza baada ya maambukizi ya VVU kuendelea kuongezeka kwa kasi katika nchi nyingi ikiwemo Uganda ambayo awali ABC ilionyesha mafanikio.Changamoto kubwa zilizo jitokeza ni pale unapomshauri mtu aache kufanya ngono pasipo kumfundisha mbinu mbadala hasa anapojisikia kufanya ngono.Mimi naamini kuwa hakuna mtu anayeamua kufanya ngono tu kama vile mtu ulivyozoea kuvaa nguo.Ili mtu afikie uamuzi wa kufanya ngono ni lazima kuwepo na msisimko fulani mwilini, kwa maana hiyo pale mtu anapopata msisimko huo ambao pengine anaweza kushindwa kuukabili hadi aamue kufanya ngono na unapomwambia aache au asubiri pasipo kumshauri nini cha kufanya anapopata haja hii,utakuwa hujamshawishi.Hapa sisemi mtu hawezi kuacha kufanya ngono bali naongelea ukweli na hali halisi ilivyo.Changamoto nyingine katika suala hilihili ni pale unapomshauri binti wa Uswahilini kwa mfano,binti ambaye hajaenda shule ama hana ajira maalumu na wazazi wake maisha yao ndiyo hayo.Binti huyu anahitaji kupendeza kwa mavazi,anahitaji chakula,anahitaji vipodozi na kwenda saluni na pengine anahitaji kuwa na simu na matumizi mengine kedekede ya mabinti hasa wa kizazi hiki cha ‘dot com’ na ambapo ‘option’ pekee ya kuvipata vyote hivyo ni kwa kufanya ngono ili apate fedha ya kujipatia mahitaji yake yote ,je unadhani binti huyu ukimwambia aache kufanya ngono asubiri pasipo kumpa mbinu mbadala za kujipatia mahitaji yake ,unafikiri ataacha kweli?.Hapa tunajifunza kwamba mapambano ya Ukimwi si kumwambia mtu aache kufanya ngono tu bali kumpa mbinu mbadala  za kufurahi na mpenzi wake pasipo kufanya ngono,kumfundisha mtu jinsi ya kuzitawala hisia zake na kuzishilikisha sekta zote kikamilifu ili kumwezesha kila mmoja kuwa na njia dhabiti ya kujipatia mahitaji yake na kuondoa umasikini.
  Changamoto pia zimejitokeza katika suala la watu kuwa waaminifu kwa mpenzi mmoja.Fikiria migogoro inayojitokeza kati ya wapenzi na wanandoa.Kwa mfano iwapo mwana ndoa mmoja atagundua mapungufu fulani kwa mwenzake mfano njia  ya kufanya mapenzi na wakishindwa kuwa tayari kuongea kwa uwazi ili kutatua mapungufu hayo  labda kutokana na aibu,mila au hofu ya kufikiria kuwa mwenzio atakuona muhuni ni wazi kwamba utashawishika kwenda nje ya uhusiano kutafuta raha ambayo mwenzio hawezi kukupa,raha ambayo iwapo mngekuwa wawazi na kuongelea matatizo yanayojitokeza hasa wakati wa kufanya tendo la ndoa,mngeweza kutatua na kuboresha mapenzi yenu na kupelekea kuwa waaminifu zaidi. Kutoongelea matatizo katika mahusiano,migogoro kati ya wapenzi na wanandoa  na tamaa za mtu binafsi ambayo pengine ni  kutokana na makuzi  na mfumo wa maisha wa mtu aliyopitia vyote hivi vimeifanya mbinu ya kuwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja kushindwa kutekelezeka.Labda sasa kuna haja ya kuwa na wataalamu maalumu wa kushauri wapenzi wanapokuwa na migogoro katika mahusiano (Sexuality counselors) tofauti na hali ilivyo kwa sasa ambapo jukumu hilo limebaki kwa Madaktari (hasa migogoro inapohusisha mabadiliko katika afya ya mtu),Maafisa Ustawi wa jamii( ambao wanahusika zaidi mahusiano yanapovunjika ),Viongozi wa dini,Wanasaikolojia (ambao wameshirikishwa zaidi katika magonjwa ya akili) na Mahakama (pale talaka zinapohitajika).Ukweli ni kwamba kwa kuwa na washauri maalumu ya masuala ya mahusiano wakiwa na ofisi zao tulivu na kwa usiri wapenzi wataongozwa katika kujadiliana mbinu za kutatua migogoro katika mahusiano na hiyo inaweza kuboresha uaminifu kati yao.
       Changamoto kubwa zaidi zimeonekana katika matumuzi ya kondomu,mbali na kupingwa na baadhi ya madhehebu ya dini,kushindwa kujua ni umri gani sahihi wa kuanza kumfundisha kijana kuhusu matumizi ya kondomu,mtazamo hasi katika jamii pale mtu anapoonekana kabeba kondomu katika pochi au mfuko wake.Na mbaya zaidi pale mtu anaposhindwa kutumia anapofikia wakati wa  kuamua kufanya ngono.Imeonekana kwamba suala la mtu kuamua kutumia kondomu hata kama anayo katika mfuko wa suruali au pochi yake aliyoiweka pembeni mwa kitanda wakati anapotaka kufanya ngono ni gumu.Suala la kuamua kuchukua na kutumia kondomu kwa kuunyoosha tu mkono kuifikia kondomu hasa anapokuwa ‘amechemka’,pochi au suruali inaonekana kama vile ipo Marekani yeye yupo Bongo!.Ni wapenzi wangapi wanaoendelea kutumia kondomu hasa baada ya kuaminiana?.Kuna mifano mingi sana inayoonyesha kuwa njia ya ABC ina mapungufu ama walioiharalisha hawakufikiria matatizo ambayo yangeweza kujitokeza hasa katika nchi za uchumi wa aina yetu na kupelekea njia hii kutoleta mafanikio yaliyotegemewa katika kupunguza maambukizi ya VVU kwa maana hiyo ‘ABC’ kama ni kisu kimepoteza makali yake.
        Sisemi ABC isiwepo,acha iendelee kuwepo lakini sasa kuna haja ya kutafuta mbinu mpya kabisa mbali na kile kinachoitwa stadi za maisha.Suala kubwa hapa ni kumwezesha mtu kuchukua uamuzi sahihi pale anapofikiria au anapokuwa katika mazingira ya kufanya ngono.Kumwezesha mtu kutambua kwa undani faida za uamuzi wowote atakaochukua pale anapofikiria kufanya ngono.Awezeshwe kutambua thamani yake,dhumuni la mungu wake kumleta duniani,jukumu lake,malengo na matarajio yake,thamani ya mwili wake na umuhimu wa afya yake kuwa imara ili aweze kuyakabili majukumu yake kama mama au baba pale atakapoamua kuanza maisha ya ndoa.
       Mwanasaikolojia mmoja nchini Thailand aliwahi kusema, ‘Mtu anaposhindwa kutambua faida na hasara za uamuzi wake na mtu huyo kuchukua uamuzi ambao unahatarisha hatima ya maisha na afya yake,basi tayari ni mgonjwa wa akili na anahitaji kuwaona wanasaikolojia ambao hata hivyo hawatamsaidia sana kwani madhara ya uamuzi wake hayawezi kubadilishwa’.
       Tunachojifunza hapa ni kufikiri kabla ya kutenda.
Mwanamtandao

WALIMU WA SAUT WANAWALAZIMISHA WANAFUNZI WA KIKE KUFANYA NAO NGONO LA SIVYO .

Hii ni Barua iliyo tumwa kwa VC na DVCAA wa SAUT KUHUSU UDHALILISHAJI WA WANAFUNZI HASA WA MWAKA WA KWANZA

Ndugu,
'Maadili' au 'uadilifu'  ni Msingi  mkubwa sana katika Kuboresha Elimu na Kuwajenga Wataalamu wenye Maadili na Uadilifu ili kuweza kulinjenga taifa letu hili lililonyuma kimaendeleo. Ili Kupata Wahitimu walio na Maadili mema na waadilifu  katika kulitumikia taifa ni vema Wakufunzi wa Vyuo wawe na Maadili mema na Waadilifu.

Wazazi Wanapowaruhusu watoto wao kuja Vyuoni... wanakuwana IMANI Kubwa sana na Wakufunzi ,kwamba wataendeleza Malezi na Maadili mema ambayo wazazi wamewafundisha watoto wao. Miaka ya Nyuma Mwanafunzi mmoja aliandika Makala katika Gazeti la Familia, inayohusu 'Jinsi  Wakufunzi wanavyowadhalilisha Watoto wa kike katika Vyuo Vikuu wakitishia Kuwafelisha iwapo hawatakubali kufanya nao Mapenzi'. Kwa bahati mbaya Gazeti hilo lilipotea baada ya Muda mfupi na halikuendelea kuchapishwa.. Wizara ya Sayansi na Elimu ya Juu ikakaa kimya labda kwa kuwa hawakuweza kulisoma..... Mimi ninayo nakala ya Makala hiyo.
Baada ya Hapo mimi pamoja na Wadau wengine wa Mapambano ya Udhalilishwaji na Unyanyasaji dhidi ya Wanawake tulianza kufanya Utafiti kuhusu hali hiyo... Na baada ya Muda Mabinti wengi sana waliwasilisha malalamiko yao kwetu kuhusu Kuombwa Unyumba na Wakufunzi na kutishiwa kufelishwa mitihani iwapo hawatakubali.

Nichukue nafasi hii  Kwa niaba ya Timu ya Marafiki wa Maisha Tanzania kukufahamisha kuwa Hadi wiki iliyopita tumepokea Malalamiko Mengi sana ya Wanafunzi kutoka Katika Chuo Chako.
Malalamiko Mengi yanatoka kwa Vijana wa Mwaka wa Kwanza hasa wakiwalalamikia Wakufunzi Vijana. Mfano ni Mkufunzi wa somo la Sociology  katika Kampasi ya Mtwara ambaye ni kijana na hana Muda mrefu katika Kazi hii. Mkufunzi huyu amakuwa akiwasumbua wanafunzi kwa kuwaita ofisini na kuwatongoza huku akitishia kuwafelisha mitihani iwapo hawatamkubali..na bahati nzuri tunayo recording ya Manongezi yake na baadhi ya Wanafunzi wa kike.Tunayo pia malalamiko ya Wakufunzi wa BAED Katika Kampus ya Mwanza na Malalamiko mengine mengi tu

Natambua kuwa moja wapo ya Vigezo vya kuwachagua Wakufunzi vyuo vyenu ni kuwa lazima Mwombaji awe Mwadilifu na mwenye kufuata maadili ya Ualimu  na iwapo hazinagatii hili na kuwachagua wakufunzi kwa kuangalia vigezo vingine kama ujamaa na undungu (japo siamini kuwa mnafanya hivyo). Kama hiyo ndivyo ilivyo ninyi kama wakuu wa vyuo hivi mnalo jukumu la kusimamia maadili haya.
Jina la chuo ni Mtakatifu Agustiono, Maisha ya Mtakatifu huyu yalijaa uadilifu na ndiyo maana Vatikan ikaamua kumweka katika maisha ya Utakatifu.. Tulitegemea pia wakunfunzi wa Chuo wawe watakatifu kimaadili.
 Tukiangalia Mission na Vision yenu
VISION ya SAUT
When the Catholic Bishops of Tanzania decided to extend the Church’s services to the provision of higher education they envisioned a training that would not only impart academic and professional skills but also that would inculcate values of civic and social learning and ethics, such as acquisition of national identity, cultural norms, political growth and responsible citizenship. Thus the Church’s vision is the holistic development of a person and respect for human dignity.

St. Augustine University of Tanzania strives at:
  • being a centre of excellence by providing a high quality of education, research and public service;
  • promoting the pursuit and defence of truth with transparency and honesty, and service with competence and dedication;
  • developing a sense of caring for personal and community property;
  • a holistic development of the person by providing sound knowledge, higher analytical ability and commitment to generous service and respect for humankind.
  • Conscious of man’s orientation towards God and neighbour and fostering an ethical and service-oriented approach in its academic and professional training, St. Augustine University of Tanzania fulfils its goal by preparing persons well equipped to contribute to the ideals of social, economic and political development.
Iwapo Wakufunzi wenu ndiyo Chanzo cha kuvunja MISSION na VISION Zetu je Watanzania wataaminije kuwa Vision na Mission zenu ni za Kweli?
Kwa Kuanzia Tunawasilisha maombi kwenu hasa kumhamisha mkufunzi wa BAS kwa Mwaka wa Kwanza katika Kampus ya Mtwara. Kwa kuwa awali alikuwa na masomo matatu na sasa  ameachiwa masomo mawili baada ya kuletwa kwa  Mkufunzi mwingine.. Ni vema jukumu hilo akaachiwa mkufunzi huyu mgeni
Tunajua Kuna risk ya Kufelishwa Mitihani kwa Wanafunzi walioleta malalamiko yao lakini tumejiweka vizuri kupambana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kwenda mahakamani ili mitihani yao isahihishwe na wakufunzi watakaoteuliwa na mahakama (Iwapo watfelishwa na Mkufunzi huyu na ushahidi wa recordings na Picha tulizonazo zatosha kabisa.... Lakini tusingependa kufikia huko. Ni Vema uongozi wa chuo Uchukue hatua za haraka kuhakikisha kuwa wakufunzi wanakuwa na maadili na kwa kuwahamisha wale wanaolalamikiwa na kuwapa Maonyo.

Tunatarajia kuwa uongozi  wenu utachukua hatua  muafaka kutatua hali hii. Tunaendelea Pia Kuwasiliana na Cecylia Malamsha, Ass. Dean wa Mtwara Kampus ambaye hata hivyo bado hajatoa msaada sana pengine ni kwa sababu hana mamlaka ya kumhamisha Mkufunzi

Tutaendelea kuwapa taarifa za malalamiko ya Wanafunzi kwani lengo letu ni kuahikisha tunakuwa na vyuo vikuu vyenye maadili sahihi
Na tutatumia Mfumo wa Utoaji HAKI nchini ambayo ni Mahakama iwapo hamtachukua hatua za Haraka


Wenu Katika Udumishaji wa Maadili Nchini, 
M/Kiti
MTANDAO WA WADAU WA MAADILI NCHINI